Ufungaji

React imeundwa tangu mwanzo ili uweze kuitumia unapotaka. Unaweza kutumia React kidogo au nyingi kadri unavyohitaji. Iwe unataka kupata ladha ya React, ongeza mwingiliano fulani kwenye ukurasa wa HTML, au uanzishe programu changamano inayoendeshwa na React, sehemu hii itakusaidia kuanza.

Jaribu React

Huhitaji kusakinisha chochote ili kucheza na React. Jaribu kuhariri katika mazingira haya ya majaribio!

function Greeting({ name }) {
  return <h1>Habari, {name}</h1>;
}

export default function App() {
  return <Greeting name="dunia" />
}

Unaweza kuihariri moja kwa moja au kuifungua kwenye kichupo kipya kwa kubonyeza kitufe cha “Fork” kwenye kona ya juu kilia.

Kurasa nyingi katika hati za React zina mazingira ya majaribio kama hii. Nje ya hati za React, kuna mazingira ya majaribio mengi mtandaoni vinavyotumia React: kwa mfano, CodeSandbox, StackBlitz, or CodePen.

Ili kujaribu React kwenye kompyuta yako download this HTML page. Ifungue kwenye kihariri chako na kwenye kivinjari chako!

Kuunda Programu ya React

Ikiwa ungependa kuanzisha programu mpya ya React, unaweza kuunda programu ya React kwa kutumia mfumo uliopendekezwa.

Unda Programu ya React kutoka Mwanzo

Ikiwa mfumo haufai mradi wako, unapendelea kuunda mfumo wako mwenyewe, au unataka tu kujifunza misingi ya programu ya React unayoweza kuunda programu ya React kuanzia mwanzo.

Ongeza React kwa mradi uliopo

Ikiwa ungependa kujaribu kutumia React katika programu yako iliyopo au tovuti, unaweza kuongeza React kwa mradi uliopo.

Note

Nafaa kutumia Create React App

Hapana. Create React App imeacha kutumika. Kwa maelezo zaidi, angalia Machweo Create React App.

Hatua zinazofuata

Nenda kwenye mwongozo wa Kuanza Haraka kwa ziara ya dhana muhimu zaidi za React utakazokutana nazo kila siku.