Quick Start
Karibu kwenye nyaraka za React! Ukurasa huu utakupa utangulizi wa 80% ya dhana za React utakazotumia kila siku.
You will learn
- Jinsi ya kuunda na kupangilia vipengele
- Jinsi ya kuongeza markup na mitindo
- Jinsi ya kuonyesha data
- Jinsi ya kutoa hali na orodha
- Jinsi ya kujibu matukio na kusasisha skrini
- Jinsi ya kushirikisha data kati ya vipengele
Kuunda na Kupangilia Vipengele
Programu za React zinatengenezwa kwa vipengele. Kipengele ni sehemu ya UI (User Interface) yenye mantiki na mwonekano wake. Kipengele kinaweza kuwa kidogo kama kitufe, au kikubwa kama ukurasa mzima.
Vipengele vya React ni functions za JavaScript zinazorejesha markup:
function MyButton() {
return (
Mimi ni kitufe
}Sasa kwa kuwa umetangaza MyButton, unaweza kukipangilia ndani ya kipengele kingine:
export default function MyApp() {
return (
Karibu kwenye programu yangu
<MyButton />
}Angalia kuwa <MyButton /> huanza na herufi kubwa. Hii ndiyo inavyoonyesha kuwa ni kipengele cha React. Majina ya vipengele vya React lazima yaanze na herufi kubwa, wakati vitambulisho vya HTML vinapaswa kuwa na herufi ndogo.
Tazama matokeo:
function MyButton() { return (  I'm a button  ); } export default function MyApp() { return (
Welcome to my app
<MyButton />
Keywords za export default zinaonyesha kipengele kikuu kwenye faili. Ikiwa haujafahamiana na baadhi ya sintaksia ya JavaScript, MDN na javascript.info zina rejea nzuri.
Kuandika Markup ukitumia JSX
Sintaksia ya markup uliyokutana nayo hapo juu inaitwa JSX. Ni hiari, lakini miradi mingi ya React hutumia JSX kwa urahisi wake. Zana zote tunazopendekeza kwa vitumizi ya ndani zinawezesha JSX moja kwa moja.
JSX ina umanani wa juu zaidi kuliko HTML. Unapaswa kufunga vitambulisho kama
. Kipengele chako pia hakiwezi kurudisha vitambulisho vingi vya JSX bila kuvifungisha katika mzazi wa pamoja, kama
au kifungashio tupu <>...</>:
function AboutPage() {
return (
Kuhusu
Habari za hapa.
Hali yako?
}Ikiwa una HTML nyingi ya kuhamisha kwenye JSX, unaweza kutumia kibadilishaji cha mtandaoni.
Kuongeza mitindo
Katika React, unaelezea darasa la CSS kwa kutumia className. Inafanya function sawa na sifa ya HTML class:
Kisha unaandika sheria za CSS kwa ajili yake kwenye faili tofauti ya CSS:
/* Katika CSS yako */
.avatar {
border-radius: 50%;
}React haielekezi jinsi ya kuongeza faili za CSS. Katika hali rahisi, utaongeza kitambulisho cha <link> kwenye HTML yako. Ikiwa unatumia zana ya ujenzi au fremu, rejea nyaraka zake ili kujifunza jinsi ya kuongeza faili ya CSS kwenye mradi wako.
Kuonyesha data
JSX hukuruhusu kuweka markup ndani ya JavaScript. Mabano ya curly hukuruhusu “kurudi kwenye JavaScript” ili uweze kuweka kigezo kutoka kwenye msimbo wako na kukionyesha kwa mtumiaji. Kwa mfano, hii itaonyesha user.name:
return (
{user.name}
);Unaweza pia “kurudi kwenye JavaScript” kutoka kwa sifa za JSX, lakini lazima utumie mabano ya curly badala ya nukuu. Kwa mfano, className="avatar" hupitisha kamba ya "avatar" kama darasa la CSS, lakini src={user.imageUrl} husoma thamani ya kigezo cha JavaScript user.imageUrl, kisha hupitisha thamani hiyo kama sifa ya src:
return (
);Unaweza kuweka maonyesho magumu zaidi ndani ya mabano ya curly ya JSX pia, kwa mfano, string concatenation:
const user = { name: 'Hedy Lamarr', imageUrl: 'https://i.imgur.com/yXOvdOSs.jpg', imageSize: 90, }; export default function Profile() { return ( <>
{user.name}
Katika mfano ulio hapo juu, style={{}} si sintaksia maalum, bali ni {} ya kawaida ya kitu (object) ndani ya mabano ya curly ya style={ } ya JSX. Unaweza kutumia sifa ya style pale ambapo mitindo yako inategemea vigezo vya JavaScript.
Utoaji Masharti
Katika React, hakuna sintaksia maalum ya kuandika masharti. Badala yake, utatumia mbinu zile zile unazotumia wakati wa kuandika msimbo wa kawaida wa JavaScript. Kwa mfano, unaweza kutumia kauli ya if ili kujumuisha JSX kwa masharti:
let content;
if (isLoggedIn) {
content = <AdminPanel />;
} else {
content = <LoginForm />;
return (
{content}
);Ikiwa unapendelea msimbo mfupi, unaweza kutumia opereta ya masharti ?. Tofauti na if, inafanya function ndani ya JSX:
{isLoggedIn ? (
<AdminPanel />
<LoginForm />
Wakati hauhitaji tawi la else, unaweza pia kutumia sintaksia fupi ya kimantiki &&:
{isLoggedIn && <AdminPanel />}
Njia hizi zote pia hufanya function kwa maalumisha sifa kwa masharti. Ikiwa hujafahamiana na baadhi ya sintaksia hii ya JavaScript, unaweza kuanza kwa kila mara kutumia if...else.
Utoaji wa Orodha
Utatumia vipengele vya JavaScript kama for loop na array map() function ili kutoa orodha za vipengele.
Kwa mfano, tuseme una safu (array) ya bidhaa:
const products = [
{ title: 'Kabeji', id: 1 },
{ title: 'Kitunguu Saumu', id: 2 },
{ title: 'Tofaa', id: 3 },
];Ndani ya kipengele chako, tumia function ya map() kubadilisha safu ya bidhaa kuwa safu ya vipengele vya
const listItems = products.map(product =>
{product.title}
return (
{listItems}
);Angalia jinsi
inavyokuwa na sifa ya key. Kwa kila kipengele kwenye orodha, unapaswa kupitisha kamba au namba inayotambulisha kwa kipekee kipengele hicho miongoni mwa ndugu zake. Kwa kawaida, key inapaswa kutoka kwenye data yako, kama vile kitambulisho cha hifadhidata. React hutumia funguo hizi kufuatilia kilichotokea ikiwa utaongeza, kufuta, au kupanga upya vipengele.
); return (
{listItems}
Kujibu matukio
Unaweza kujibu matukio kwa kutangaza functions za handler za matukio ndani ya vipengele vyako:
function MyButton() {
function handleClick() {
alert('You clicked me!');
return (
Click me
}Angalia jinsi onClick={handleClick} haina mabano mwishoni! Usiiite event handler moja kwa moja: unahitaji tu kuipitisha chini. React itaendesha handleClick wakati mtumiaji atabofya kitufe.
Kusasisha skrini
Mara nyingi, utataka kipengele chako “kikumbuke” taarifa fulani na kuionesha. Kwa mfano, labda unataka kuhesabu ni mara ngapi kitufe kimebofya. Ili kufanya hivyo, ongeza hali (state) kwenye kipengele chako.
Kwanza, leta useState kutoka React:
import { useState } from 'react';Sasa unaweza kutangaza variable ya hali ndani ya kipengele chako:
function MyButton() {
const [count, setCount] = useState(0);
// ...Utapata mambo mawili kutoka kwa useState: hali ya sasa (count), na function inayokuwezesha kuibadilisha (setCount). Unaweza kuyapa majina yoyote, lakini desturi ni kuandika [something, setSomething].
Mara ya kwanza kitufe kinapoonyeshwa, count itakuwa 0 kwa sababu uliipitisha 0 kwenye useState(). Wakati unataka kubadilisha hali, piga setCount() na upitishe thamani mpya kwake. Kubofya kitufe hiki kutaongeza kaunta:
function MyButton() {
const [count, setCount] = useState(0);
function handleClick() {
setCount(count + 1);
return (
Umebofya mara {count}
}React itaita tena function ya kipengele chako. Wakati huu, count itakuwa 1. Kisha itakuwa 2. Na kadhalika.
Ikiwa utaonyesha kipengele kimoja mara nyingi, kila moja kitapata hali yake. Bofya kila kitufe kando kando:
import { useState } from 'react'; export default function MyApp() { return (
Counters that update separately
<MyButton /> <MyButton />
); } function MyButton() { const [count, setCount] = useState(0); function handleClick() { setCount(count + 1); } return (  Clicked {count} times  ); }
Kumbuka jinsi kila kitufe “kinakumbuka” hali yake ya count na hakiathiri vitufe vingine.
Kutumia hooks
Functions zinazooanza na use zinaitwa Hooks. useState ni Hook ya kujengwa inayotolewa na React. Unaweza kupata Hooks nyingine zilizojengwa kwenye marejeleo ya API. Pia unaweza kuandika Hooks zako mwenyewe kwa kuchanganya zile zilizopo.
Hooks huwa restrictive kuliko functions nyingine. Unaweza tu kuita Hooks juu ya vipengele vyako (au Hooks nyingine). Ikiwa unataka kutumia useState katika hali au mzunguko, toa kijenzi kipya na kueka hapo.
Kushirikisha data kati ya vipengele
Katika mfano wa awali, kila MyButton ilikuwa na hali yake ya kujitegemea count, na kila kitufe kilipo bonyezwa, count ya kitufe kilichobonyezwa pekee ndiyo ilibadilika:
Awali, kila hali ya count ya MyButton ni 0
Kijenzi cha kwanza cha MyButton kinasasisha count yake hadi 1
Hata hivyo, mara nyingi utahitaji vijenzi kushirikiana data na kila wakati kubadilika pamoja.
Ili kufanya vijenzi vyote viwili vya MyButton kuonyesha count sawa na kubadilika pamoja, unahitaji kuhamisha hali kutoka kwa vitufe vya kibinafsi “juu” hadi kijenzi cha karibu kinachovijumuisha vyote.
Katika mfano huu, ni MyApp:
Awali, hali ya count ya MyApp ni 0 na inapasiwa kwa watoto wote wawili
Kwa kubonyeza, MyApp inasasisha hali yake ya count hadi 1 na kuipasi kwa watoto wote wawili
Sasa unapobonyeza kitufe chochote, hali ya count katika MyApp itabadilika, ambayo itabadilisha hali ya count katika kila MyButton. Hivi ndivyo unavyoweza kuonyesha hili kwa msimbo.
Kwanza, hamisha hali kutoka MyButton hadi MyApp:
export default function MyApp() {
const [count, setCount] = useState(0);
function handleClick() {
setCount(count + 1);
return (
Counters that update separately
<MyButton />
<MyButton />
function MyButton() {
// ... tunahamisha msimbo kutoka hapa ...
}Kisha, pitisha hali kutoka MyApp hadi kila MyButton, pamoja na handler ya kubonyeza ya pamoja. Unaweza kupitishia habari kwa MyButton ukitumia mabano ya JSX, kama vile ulivyofanya awali na lebo zilizojengwa kama :
export default function MyApp() {
const [count, setCount] = useState(0);
function handleClick() {
setCount(count + 1);
return (
Counters that update together
<MyButton count={count} onClick={handleClick} />
<MyButton count={count} onClick={handleClick} />
}Habari unazopitishia hivi zinaitwa props. Sasa kipengele cha MyApp kina hali ya count na mshughulikiaji wa tukio handleClick, na inapasia zote mbili kama props kwa kila kitufe.
Mwisho, badilisha MyButton ili kusoma props ulizopitishia kutoka kwa mzazi wake:
function MyButton({ count, onClick }) {
return (
Clicked {count} times
}Unapobonyeza kitufe, handler ya onClick inawashwa. Prop ya onClick ya kila kitufe ilipangwa kwa function ya handleClick ndani ya MyApp, hivyo msimbo ndani yake unafanya function. Kazi hiyo inaita setCount(count + 1), ikiongeza hali ya count. Thamani mpya ya count inapaswa kama prop kwa kila kitufe, hivyo vyote vinaonyesha thamani mpya. Hii inaitwa “kupandisha hali”. Kwa kuhamisha hali juu, umeishirikisha kati ya vipengele.
import { useState } from 'react'; export default function MyApp() { const [count, setCount] = useState(0); function handleClick() { setCount(count + 1); } return (
Counters that update together
<MyButton count={count} onClick={handleClick} /> <MyButton count={count} onClick={handleClick} />
); } function MyButton({ count, onClick }) { return (  Clicked {count} times  ); }
Hatua Zifuatazo
Kwa sasa, unajua misingi ya jinsi ya kuandika msimbo wa React!
Angalia Mafunzo ili kufanya mazoezi na kujenga mini-app yako ya kwanza na React.